Taasisi ya Volunteers In Development (VID) inayosaidia watoto yatima wa
majumbani wajane na wasiojiweza, iliyopo jijini Dar es Salaam, imewataka
wadau mbalimbali kujitokeza katika zoezi la ujenzi wa kituo cha kijamii
ambacho kitakuwa msaada mkubwa wa makundi hayo.
Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa taasisi hiyo Bi. Tune Shaabani, na
kusema kuwa jengo hilo litakuwa na huduma mbalimbali zitakazo nufaisha
jamii wanayoisaidia ikiwa ni pamoja na elimu ya awali, elimu ya ujuzi,
madarasa ya kompyuta.
“Jengo hili litakuwa na nursary clasess, computer clases na masuala ya
ujasiriamali. Tunawaomba wadau watuunge mkono katika hili kwani si lazima
mtu atupatie fedha moja kwa moja bali anaweza kuchangia mahitaji ya ujenzi
kama simenti, nondo na vifaa mbalimbali vya ujenzi” amesema.
Kwa upande wake Khadija Sheikh amesema, ujenzi wa jengo hilo utakuwa
kama kivuli kwani utasaidia taasisi kupunguza kuomba misaada kwa wadau
mbalimbali kwani kitakachopatikana kutokana na shughuli za kila siku,
utawezesha kazi mbalimbali zinazofanyika kutimia.
Taasisi ya Volunteers In Development (VID) ni taasisi na shirika lisilo la
kiserikali lililo chini ya wanawake ambalo lilisajiliwa rasmi mwaka 2014. VID
imejikita kuwasaidia watoto yatima wa majumbani, wajane, watu wasiojiweza
ili kuleta maendeleo endelevu katika jamii zetu na kuondoa pengo la usawa.
Latest news delivered right to your inbox!
Leave a Reply