Taasisi ya Volunteers In Development (VID) inayosaidia watoto yatima wa
majumbani, wajane na wasiojiweza, wamewataka wadau mbalimbali
kujitokeza kuisaidia jamii hiyo ili kuleta maendeleo mazuri kwa wote.
Akizungumza katika zoezi la ugawaji wa futari na nguo za sikukuu kwa familia
za watoto yatima, Zainabu Katimba amesema kuwa bado msaada wa nje
umekuwa mdogo kumudu mahitaji ya watoto, wajane na wasiojiweza.
“Hatuna Donor wa kutuunga mkono, kwa mfano leo tupo katika zoezi la
ugawaji wa nguo za watoto, lakini ni sisi wenyewe tunaojitolea sadaqa
zimeweza kutimiza mahitaji haya” amesema.
Amesema inasikitisha kuona idadi inaongezeka kila kukich na kuna wahitaji
wengi zaidi katika jamii zetu, wanaoishi chini ya kiwango cha umaskini (below
poverty line) ingawa mpaka sasa wamemudu hao wachache.
Kila mwanzo wa mwaka taasisi inawapatia mahitaji ya shule (back to school
kits) watoto hawa ili nao wapate motisha ya kujiendeleza kielimu. Pia huwa
wanawapatia educational counseling ili kutambua na kutatua vikwazo
wanavyopitia katika masomo yao. Kwa hakika si jambo kubwa sana la
kushangaza kwa matajiri lakini kutoa ni moyo.
Latest news delivered right to your inbox!
Leave a Reply