Wazazi na walezi wa watoto yatima wa majumbani, wametakiwa kusimamia
maendeleo ya watoto yatima ili kuhakikisha wanatimiza ndoto na malengo
yao katika maisha.
Hayo yamesemwa na mshauri wa kisaikolojia Ostadhi Ismail Mussa wakati
wa zoezi la ugawaji wa vifaa vya shule kwa watoto yatima zaidi ya 300 toka
mkoa wa Dar es Salaam na Pwani.
“VID imechukua nafasi ya mzazi kwa kuhakikisha upatikanaji wa mahitaji yote
ili watoto waweze kwenda shule, kilichobaki ni wazazi au walezi kusimamia
vema watoto kutimiza malengo yao”.
“Bahati nzuri nimetoka katika tukio kama hili muda si mrefu, ila hapa nimekuta
utofauti mkubwa sana na huko kwanzi mtoto anatoka akiwa kamili kwa kupata
mahitaji yote” amesema.
Kwa upande wake Meneja wa VID Kasimu Haruna amesema taasisi
itasimamia vema upatikanaji wa taarifa na maendeleo mzuri kwa watoto hao,
na itawachukulia hatua kali wazazi wote ambao watashindwa kuendana na
mahitaji ya taasisi.
Nao baadhi wa walezi wa watoto yatima wameishukuru sana VID kwa
msaada wanaoutoa, kwani umewainua pakubwa kumudu gharama za elimu
na kuwataka baadhi ya walezi kutimiza mahitaji yanayohitajika na kufuata
vema kanuni na taratibu za taasisi.
Latest news delivered right to your inbox!
Leave a Reply